H5P activities list
This book includes 20 H5P activities. Only those which have been inserted into book content will be included if the book is cloned.
ID | Title | Activity type | Show/Hide |
---|---|---|---|
1 | Msamiati wa Dini | Dialog Cards | |
Flashcards Use the flashcards to practice your understanding of key vocabulary related to religion. dini 9/10 Uislamu 14 Card 1 of 30 | |||
2 | Dini | Multiple Choice | |
dini 9/10
| |||
3 | Quiz set on religious vocab | Question Set | |
4 | Supportive minimal vocalizations | Mark the Words | |
Post-reading exercise 1 In the following excerpt from Katrina's interview with Maliki, use your mouse to select the supportive minimal vocalizations that both speakers use to keep the conversation going. MALIKI; Sawa? KATRINA; Eh, sasa inarekodi. MALIKI; Mimi naitwa Maliki Adili Suleiman. KATRINA; A! Ni Maliki, si Malik? MALIKI; A-a. Malik ni kifupi tu. KATRINA; Sawa. MALIKI; Eeh, lakini ni Maliki. Mimi natokea visiwani Zanzibar. KATRINA; Kisiwa kipi? MALIKI; Unguja. KATRINA; Sehemu gani? MALIKI; Kaskazini Unguja. Inaitwa Mwanda. Nimezaliwa mwaka elfu moja mia tisa sabini na tisa. KATRINA; O! Ni mdogo wangu! @ MALIKI; @Ndiyo. @@@ KATRINA; @@@ MALIKI; Eh, nina miaka thelathini thelathini. Ya,exactly thelathini thelathini. KATRINA; Umeoa? MALIKI; Mimi nilioa, lakini sasa niko mwenyewe. Tumetengana na mwanamke. Na nina mtoto, na nimesoma kuleprimary hadi sekondari, lakini bahati mbaya nilitoka katika familia maskini, hawakuweza kuniendeleza kimasomo. Nikatoka hapo nikaomba tena kusoma, wazazi wangu wakaniambia, “kwa kweli uwezo sisi hatuna kama unavyotuona ni maskini.” Basi nikajitahidi mwenyewe, nikaanza kufanya kazi hapa na pale. Nikapata pesa kidogo, nikaingia chuo, ingawa vile vile kumaliza ilikuwa ni taabu, kwa sababu sikuwa na pesa ya kutosha. Lakini— KATRINA; Ilikuwa chuo cha aina gani? MALIKI; Nitourism . Chuo cha utalii. KATRINA;: Mmhh… MALIKI; Baadaye nikaacha tena chuo. Nikakaa tena mitaani.And then nikarudi tena chuo. Nikamaliza masomo. Nikaanza kazi kwenye hoteli moja inaitwa Breezes Beach Club. Nifive star . KATRINA; Mmhh. MALIKI; Iko Unguja. Nilifanya kazi hapo kwa muda wa miaka mitatu. Kutoka hapo nikaenda kwenye hoteli nyingine. Inaitwa Pwani Ocean Station. Nikafanya kwa mwaka mmoja. Kipindi hiko tayari nishakuwa na mwanamke. Wakati naacha kazi Pwani Ocean nikaja hukumainland ,I mean Dar es Salaam. Nikafanya kazi kwenye hoteli mmoja inaitwa Kilimanjaro Kruger Hotel. KATRINA; Mm. [...] KATRINA; Una maswali yo yote juu ya maisha yangu au? MALIKI; Ya. KATRINA; Kabla ya kuanza na hadithi? MALIKI; Ya, nitapenda mimi nijue kidogo. KATRINA; Haya. MALIKI; Maisha yako yako vipi? KATRINA; Haya. Mimi nilizaliwa Marekani, jimbo la New York. MALIKI; Ndiyo. KATRINA; Katika mji mkubwa wa New York. MALIKI; Sawa. KATRINA; Lakini nilipokuwa na miaka mitano hivi tulihamia jimbo la Massachusetts, ambapo babangu alizaliwa. Kwa sababu mamake alifariki, na tulienda kumtunza babake ambaye alikuwa mzee sana. MALIKI; Ndiyo. KATRINA; Na nilikuwa mtoto pekee wa wazazi wangu. MALIKI; Ndiyo. KATRINA; Kwa hiyo tuliondoka mji mkubwa tukaenda kijijini. Kijiji hicho kilikuwa na watu elfu nne tu. Nafikiri. Na baada ya miaka michache wazazi wangu wangu walitengana. Kwa hivyo mimi na mama yangu tulihama. Tukaenda jimbo lingine, lakini baada ya mwaka mmoja au miwili hivi tulirudi jimbo la Massachusetts ili nikae karibu na babangu. MALIKI; Ndiyo. KATRINA; Na baada ya kumaliza shule ya sekondari nilihamia pekee yangu jimbo la Iowa, kwenda chuo kikuu MALIKI; Ndiyo. KATRINA; Na wakati wa chuo kikuu niliamua kwenda Afrika, kusoma kwa nusu ya mwaka. Nikaenda Zimbabwe. Nilianza kujifunza lugha ya Kishona. MALIKI; Ndiyo. KATRINA; Na niliamua kuendelea na fasihi za Kiafrika ama lugha za Kiafrika, hasa Kishona. Lakini nilipofika chuo kikuu kingine ili kupata digrii za pili na tatu, profesa wa Kishona alikuwa amestaafu mwaka huo. Kwa hivyo walimu wengine walisema “A, itabidi usome Kiswahili badala ya Kishona.” MALIKI; @ KATRINA; Nikaanza Kiswahili, lakini sikuvutiwa sana nacho kwa sababu nilikuwa sijafika Tanzania au Kenya. MALIKI; A, ndiyo. KATRINA; Lakini baada ya miaka miwili ya kusoma Kiswahili nilipata nafasi ya kuja Tanzania. Nilikaa Unguja kwa wiki nane, pamoja na familia ya Waislamu. Na nilisoma Kiswahili pale Taasisi. MALIKI; Ndiyo. KATRINA; Halafu baada ya hapo nimerudi mara nyingi. Sasa kila mwaka au miaka miwili narudi. MALIKI; Ndiyo. KATRINA; Naenda kuwatembelea familia MALIKI; Mmm. KATRINA; ya Unguja. Au nakuja Dar es Salaam. Kwa hiyo nina marafiki hapa. Vizuri! Sio. Ulisahau! | |||
5 | Pre-reading exercises for "Maliki" interview | Documentation Tool | |
Pre-reading exercises Pre-reading Exercise 1 Pre-reading Exercise 2 Document Export More information Pre-reading Exercise 1 This exercise, and the next one, require you to fill in your answers. At the end, you will be able to export your answers to print, save, and/or submit to your teacher or conversation partner. Jina lako Think about what you already know about interviews in your own language and culture. 1. How would you distinguish between a conversation (mazungumzo) and an interview (mahojiano)? Make a list, in Swahili, the features you can think of for each type of communication. 2. Do you expect to find the same features in a Swahili interview? Why or why not? 3. If you are a classroom learner, compare your list with your classmates. Which features do you agree on? More information Pre-reading Exercise 2 1. Discourse analysts use the term supportive minimal vocalizations to refer to utterances where a speaker utters minimal responses like mmm or yeah or laughs, where the purpose is not to express a literal meaning but rather to show that they are listening or help the conversation continue. Think about how people in your culture usually signal that they are listening during a conversation or interview. Make a list of at least 5 words or sounds people use to simply help the conversation in English. 2. Do you expect to find the same supportive minimal vocalizations in a Swahili interview? Make a list of those you already know in Swahili and/or what you would expect the equivalents to be. More information Document Export Well done! On this page you can choose to export your answers to print, save, and/or submit to your teacher or conversation partner. Create document One or more required input fields need to be filled. | |||
6 | Post-reading activity for "Maliki" interview | Documentation Tool | |
Documentation tool Post-reading exercise 2 Document Export Post-reading exercise 2 This exercise requires you to fill in your answers. At the end, you will be able to export your answers to print, save, and/or submit to your teacher or conversation partner. Jina lako How are the supportive minimal vocalizations that Maliki and Katrina used similar to or different from what you predicted in the pre-reading activity? Did you notice any differences between those Katrina used and those Maliki used? Do you have any guesses as to why they might have differed? Which do you think you will use when you conduct an interview in Swahili? Why? More information Document Export Well done! On this page you can choose to export your answers to print, save, and/or submit to your teacher or conversation partner. Create document One or more required input fields need to be filled. | |||
7 | Comprehension questions for Maliki interview | Single Choice Set | |
Swali 1 katika maswali 8 Kati ya Katrina na Maliki, yupi ana umri mkubwa?
Je, Maliki ana mke sasa?
Maliki anakaa wapi sasa?
Maliki anafuata dini gani?
Katrina anatoka wapi?
Katrina alijifunza lugha gani ya Kiafrika kwanza?
Ukitaka kufanya mahojiano na Maliki, utamtafuta wapi?
Majibu
| |||
8 | Post-re-reading activity for Maliki interview | Documentation Tool | |
Documentation tool Post-reading Exercise 4 Document Export Post-reading Exercise 4 This exercise requires you to fill in your answers. At the end, you will be able to export your answers to print, save, and/or submit to your teacher or conversation partner. Jina lako Although the purpose of the interview was to discuss Popobawa, it goes on for 87 lines without either Katrina or Maliki mentioning Popobawa. What do you think was the purpose of this portion of the interview? What did you learn about Maliki's religious beliefs? Why do you think Katrina asked Maliki, "Wewe ni Mwislamu?" What are some other ways she might have asked about his religious beliefs, and how might the form of the question influence his possible answers? More information Document Export Well done! On this page you can choose to export your answers to print, save, and/or submit to your teacher or conversation partner. Create document One or more required input fields need to be filled. | |||
9 | Al Fatiha with hotspots | Image Hotspots | |
10 | Understanding Al Fatiha | Fill in the Blanks | |
Jaza nafasi Sura ya kwanza ya Korani iko katika juzuu ya . Ina saba. Mtume Mohamed alikuweko | |||
11 | Discussion questions about Al Fatiha | Documentation Tool | |
Documentation tool Discussion questions Document Export Discussion questions This exercise requires you to fill in your answers in Swahili. At the end, you will be able to export your answers to print, save, and/or submit to your teacher or conversation partner. Jina lako Is there any text (a religious verse; or a poem, perhaps) that you have memorized? Why and how did you learn it? What does it mean to you? Based solely on the text of "Al Fatiha" (ignoring anything else you may know about Islam for the moment), how do you think Muslims conceptualize God and Islam? More information Document Export Well done! On this page you can choose to export your answers to print, save, and/or submit to your teacher or conversation partner. Create document One or more required input fields need to be filled. | |||
12 | Grammar exercises from Al Fatiha | Course Presentation | |
13 | Grammar from Al Fatiha: Causatives from nouns | Course Presentation | |
14 | Stative Verbs in Al Fatiha | Course Presentation | |
15 | Reduplication | Course Presentation | |
16 | Emphatic Copula | Course Presentation | |
17 | Chat test | appear.in for Chat and Talk | |
18 | Comprehension questions for Braj and Irene conversation | Question Set | |
19 | Reading | Mark the Words | |
Bonyeza kila neno ambalo linataja kiumbe kisichoonekana. Yuko popobawa anayeingilia wanaume zaidi. Anaingilia wanaume zaidi. Na:: popobawa huyu wako kama::: watatu, sijui nizungumze yupi. Lakini kuna popobawa anayetokana na mila fulani ya kufukuza balaa la mji. Wenyeji wanafukuza balaa la mji. Wanaweza wakawa watoto wamePIgwa na ugonjwa fulani wa ajabu, ambao ni watoto mji mzima, watoto wadogo. Inaweza ikawa degedege au kukohoa, watoto unakuta w- ile imepiga mji mzima. Na hata sababu za kitaalamu zinakuwa hazielezwi. Hata madaktari wakija wakiangalia, watoto wote wameathirika. Lakini sababu za za kitaalam, kwamba kwa nini wameathirika? hazipo. Sasa inaonekana, ni kama mizimu imechukia, yaani wazee wa zamani waliokufa zamani wamechukia. Kama wamechukia, e- wakichukia hawa wazee wa zamani, ndio kunakuwa na mlipuko huo wa magonjwa. Kinachofanyika, wanakwenda kwa mama wenye watoto wadogo. Wamama wenye watoto wadogo. Lakini SI wenye umri mkubwa. Wale wasichana wasichana. Wasichana wasichana. Na haitokei mara nyingi sana, inatokea kwa nadra sana, kwa—Inatokea kwa nadra sana. Sasa hao watoto wenye wamama— wamama wenye watoto wadogo, na wenyewe ni wasichana. Wanakusanyika kwenye chini ya mti mkubwa porini, ambao wanakuwa wamekaa wengi, wanapeanapeana hadithi tu, wanaongea hivi? ili kusindikiza usiku. Na hawaambiwi kitafanyika. Hawa wanakaa, wanakaa kwa muda fulani, halafu usiku mwingi, wakati wengine wamechokachoka hivi, wengine wanaanza kusinzia, wengine wanaendelea kuongea, usiku mwingi wakiwa na watoto wao wadogo. Kunakuwa na wamama, tena watu wazima. Walio:vuka kipindi kile cha kuzaa, tena, hawawezi kuzaa tena. Kipindi kile cha hedhi imekoma. Hao wamama wa umri huo. Wanakuja kwa kunyemelea. Yaani wanakuja kinyemela bila kuwa na taarifa, halafu wanawashtua. Watajua namna yoyote ya kuwashtua, kama watapiga kelele kubwa, au watapiga mabati, au tarumbeta, ambalo inatakiwa hao waSHTUke.Yaani namna yoyote ya kushtu-, maadamu tu waSHTUke.Kitendo cha kushtuka, (IMITATES SHORTNESS OF BREATH) wakishtuka wakikimbia hivi “heehee,” wanaPIga kelele! Tayari wakiSHTUka na kupiga kelele, mji umepona. Inakuwa ndiyo dawa. Tayari mji unakuwa umepona wote. Sasa, baada ya kuwa umepona mji, kwa sababu: adhabu imekuwa ni ya watoto, sasa inategemea. Kosa linakuwa ni nini? Inawezekana wazee walichukia, baada ya kuona kwamba kuna:: shida, kwa wababa. Wakaadhibiwa watoto. Kwa hiyo watoto hasa wanapopona, wanaadhibiwa wanaume. Inakuwa kama adhabu fulani hivi. Ndio wanawaingilia. Sasa yule hakuna mtu wa kumwingoza- wa kumwongoza. Wanaadhibiwa wazee. Inawezekana kumetendeka dhambi kubwa sana ama nanii, kunanii, watu wametoka nje ya ndoa zao, wamefanya uhuni wa kutosha, wengine wamezaa na wake wa watu, watu wamepokea watoto sio wa kwao— Sasa yale matatizo ya mji yakiwa mengi, ndio inakuja adhabu hiyo kwa watoto. Ikionekana adhabu imeadhibiwa watoto, maana yake shida iko kwenye ndoa. Sasa inategemea, kosa ni la wa- akina nani? Kosa kubwa— wamama ndio wamekosea zaidi? au wababa? Kama ni wababa, ndio inakuta wanaadhibiwa, maanake inakuwa nini? Kama vile wewe ulivyojisikia raha kuingia kwa mke wa mtu, au ulijisikia vizuri, kuingia kwa mtu wa harimu wako, harimu yaani mtu ambaye hurusiwi ku- kufanya naye mapenzi. Mama yako, shangazi yako, mtu ndugu yako, dada yako— Sasa madhambi kama haya yanaleta balaa katika mji. Sasa kama wababa ndio wamekosa zaidi, mpaka watoto wakapata mlipuko wa magonjwa ule, basi wanaadhibiwa wababa. Linatokea limnyama hilo linawaingilia wanaume. E::h na mizimu, mizimu ndio inawapeleka. Linawaingilia wanaume. Linakwenda mpaka kipindi, ambacho lenyewe litajisikia kuacha au watu watagundua, eh? Watagundua ile tatizo, na kuanza kuenda kuiomba mizimu, “Jamani tusameheni. Sasa tumejua makosa yetu.” Mizimu itataka kujua kama wamejua makosa yao, wataeleza kosa. Kosa ni hili,—Kama si hilo lenyewe litaendelea. Watarudia tena, kosa ni hili,— Kama silo litaendelea, mpaka lile kosa ambalo ni lenyewe, ndio lenyewe lenyewe lenyewe mizimu itaacha. [Popobawa huyu anaitwa Mufo.] Mufo ni kama mfu. Yaani aliyekufa, ni kama mizimu yaani, ni neno linalotokana na mfu. Mufo. Inaitwa Mufo au Mfu. Inaitwa Mufo. Hii ndiyo aina ya popobawa ambayo inawaadhibu wanaume. Sasa hii, haina dawa nyingine, zaidi ya kugundua kosa. Na kama hawakugundua kosa, maana sehemu nyingine, wengine wanaweza wakaamua wababa watulie. Mtu ameingiliwa na popobawa halafu akakaa kimya. Hakueleza lakini anaugua. Anaweza kumwambia mke wake tu, “Mi naumwa.” Lakini asieleze kinachomwumiza. Sasa mwingine si hatajua? Na mwingine akafanyiwa hivyo hivyo na yeye akaamua asiseme. Litaendelea litawapitia litawapitia litawapitia, mpaka linaamua lenyewe linaacha. Shetani, labda niseme shetani, ndiyo maana yake ni “asi”, ni yule aliyeasi. Kwa hiyo shetani anaweza kuwa pepo, au anaweza kuwa mwanadamu. Au anaweza kuwa kitu yoyote. Maanake ni ile hali ya kutokubaliana na Mungu. Ndiyo shetani. Yaani kinyume cha Mungu ni shetani. Awe mwanadamu anaweza kuwa shetani. Awe pepo, awe jini, anaweza kuwa shetani. Maana yake anayetofautiana na mapenzi ya Mungu, huyo ni shetani. Unaposema jini, “jini” ni neno la Kiswahili, linalotokana lenye asili ya Kiarabu. Waarabu wa zamani walikuwa wanatumia neno “janna.” “Janna.”J A double N A Janna. “Janna” kwa Kiarabu cha zamani, ni— Maanake kilichofichika, kisichoonekana kwa urahisi, yaani kisichoonekana kwa macho ya binadamu haya, kinachoonekana kwa macho ya rohoni, au, kikionekana kwa macho ya kibinadamu, maanake kuna tukio kubwa. Kuna jambo kubwa limetokea. Hiyo. Sasa Waraabu wa zamani walikuwa hawamjui Mungu, walikuwa na miungu mingi. Walikuwa wanaabudu miungu mingi! Waarabu wa zamani, KAbla ya Uislamu. Sasa ulipokuwa ukiwaambia kuwa kuna Mungu, wanakuambia tu, “Onyesha.” Kwa sababu walikuwa na miungu yao, inaonekana ni masanamu, wanakwambia huyu mungu fulani, huyu anaitwa: labda, labda miungu ya Waarabu, kwa mfano huyu nanii “Latta,” huyu anaitwa Latta. Huyu anaitwa Manattah. Huyu anaitwa Al Uzah. Hiyo ndiyo miungu ya Waarabu ya zamani. Ilikuwa inaonekana kwa macho. Sasa ukisema habari za Mungu, Mungu, kuna Mungu. Wanakuambia, “Yuko wapi?” Haonekani. Wanasema, “Basi ni janna,” yaani ni kitu kisichoonekana kwa macho ya kawaida. Ikiwa na pamoja na upepo pia ni janna. Kitu kisichoonekana kwa macho ya kawaida ya nyama. Na: chochote ambacho ni imani, bila kuonekana, walikuwa wanakiita Janna. Yaani kitu kilichojificha. Kitu cha kiroho. Unaona eh? Sasa ikaendelea hata walipopata dini sasa wakaanza kujua kuna Mungu. Mungu mwenyewe pia walikuwa wanaita Janna. Baadaye wakafanya wakafanya marekebisho, wakaona, “M-m. “Tukisema Mungu ni janna? Lakini kuna maroho mengine mabaya mabaya, yaani ni janna, sasa tutatofautishaje kati ya janna Mungu na janna asiye mungu? na janna shetani? Kwa hiyo wakaita jini. Jini ni roho mchafu, asiyepatana na Mungu. Lakini neno lenyewe limetoka kwenye asili ya neno la Kiarabu, la kitu kilichojificha. Kisichoonekana. Sasa baada ya kujua kwamba kuna Mungu asiyeonekana, walipojua hilo, ndio wakaamua kulibadilisha neno, kuna jini, na kuna Mungu. Ambayo siyo janna, yeye sio jini. Ni Mungu tu. Ambaye ni roho asiyeonekana lakini ni mzuri. Ehe:. Kwa hiyo kuna malaika na ninii. Na [pepo]. [Pepo] ni hao maroho mabaya, ni hayo hayo maroho mabaya, [...] ni kama jini, lakini jini ingawa ina maelezo mapana kidogo. Ni roho mchafu. Ndiyo! Siyo! Ulisahau | |||
20 | Test | Documentation Tool | |
Documentation tool |