Primary Source Texts

Primary Source 2

Excerpt from an interview with “Mustafa”

The following excerpt is about an hour into my interview with Mustafa (a pseudonym), a Pentecostal leader who was formerly a Muslim sheikh. We met at the Pentecostal church where he worked. Prior to this section, he had explained his educational background within Islam and told a lengthy story about one of seventeen types of popobawa with which he was familiar. Throughout our interview he displayed an unusual level of esoteric knowledge about “the unseen world.” As I describe in my book Popobawa: Tanzanian Talk, Global Misreadings, many East African Muslims and Christians believe in spirits and demons, and people have syncretized pre-Islamic beliefs in spirits with Islamic beliefs, Arabic terminology, and biblical depictions of Satan.

I have edited the transcript slightly to remove unnecessary details.

1 KATRINA; Unaweza kuendelea na popobawa mwingine?
2 MUSTAFA; Eh ah! Wako wengi. […]
3 KATRINA; Ningependa kujua kuhusu yule ambaye anaingilia wanaume zaidi.
4 MUSTAFA; A::h. Huyu ambaye anawaingilia wanaume zaidi? Sawa. Sitakuelezea kwa uhakika sana, lakini ni kwamba yuko popobawa anayeingilia wanaume zaidi. Anaingilia wanaume zaidi. Na:: popobawa huyu wako kama::: watatu,  sijui nizungumze yupi. Lakini kuna popobawa anayetokana na mila fulani ya kufukuza balaa la mji. Wenyeji wanafukuza balaa la mji. Wanaweza wakawa watoto wamePIgwa na ugonjwa fulani wa ajabu, ambao ni watoto mji mzima, watoto wadogo. Inaweza ikawa degedege au kukohoa, watoto unakuta w- ile imepiga mji mzima. Na hata sababu za kitaalamu zinakuwa hazielezwi. Hata madaktari wakija wakiangalia, watoto wote wameathirika. Lakini sababu za za kitaalam, kwamba kwa nini wameathirika? hazipo. Sasa inaonekana, ni kama mizimu imechukia, yaani wazee wa zamani waliokufa zamani wamechukia. Kama wamechukia, e- wakichukia hawa wazee wa zamani, ndio kunakuwa na mlipuko huo wa magonjwa. Kinachofanyika, wanakwenda kwa mama wenye watoto wadogo. Wamama wenye watoto wadogo.  Lakini SI wenye umri mkubwa. Wale wasichana wasichana. Wasichana wasichana. Na haitokei mara nyingi sana, inatokea kwa nadra sana, kwa—Inatokea kwa nadra sana. Sasa hao watoto wenye wamama—  wamama wenye watoto wadogo, na wenyewe ni wasichana. Wanakusanyika kwenye chini ya mti mkubwa porini, ambao wanakuwa wamekaa wengi, wanapeanapeana hadithi tu, wanaongea hivi? ili kusindikiza usiku.
5 KATRINA; Hm.
6 MUSTAFA; Na hawaambiwi kitafanyika. Hawa wanakaa, wanakaa kwa muda fulani, halafu usiku mwingi, wakati wengine wamechokachoka hivi, wengine wanaanza kusinzia, wengine wanaendelea kuongea, usiku mwingi wakiwa na watoto wao wadogo. Kunakuwa na wamama, tena watu wazima. Walio:vuka kipindi kile cha kuzaa,  tena, hawawezi kuzaa tena. Kipindi kile cha hedhi imekoma. Hao wamama wa umri huo. Wanakuja kwa kunyemelea. Yaani wanakuja kinyemela bila kuwa na taarifa, halafu wanawashtua. Watajua namna yoyote ya kuwashtua, kama watapiga kelele kubwa, au watapiga mabati, au tarumbeta, ambalo inatakiwa hao waSHTUke.Yaani namna yoyote ya kushtu-, maadamu tu waSHTUke. Kitendo cha kushtuka, (IMITATES SHORTNESS OF BREATH) wakishtuka wakikimbia hivi “heehee,” wanaPIga kelele! Tayari wakiSHTUka na kupiga kelele,mji umepona. Inakuwa ndiyo dawa. Tayari mji unakuwa umepona wote. Sasa, baada ya kuwa umepona mji,kwa sababu: adhabu imekuwa ni ya watoto, sasa inategemea. Kosa linakuwa ni nini? Inawezekana wazee walichukia, baada ya kuona kwamba kuna:: shida, kwa wababa. Wakaadhibiwa watoto. Kwa hiyo watoto hasa wanapopona, wanaadhibiwa wanaume. Inakuwa kama adhabu fulani hivi. Ndio wanawaingilia. Sasa yule hakuna mtu wa kumwingoza- wa kumwongoza. Wanaadhibiwa wazee. Inawezekana kumetendeka dhambi kubwa sana ama nanii, kunanii, watu wametoka nje ya ndoa zao, wamefanya uhuni wa kutosha,wengine wamezaa na wake wa watu,  watu wamepokea watoto sio wa kwao— Sasa yale matatizo ya mji yakiwa mengi, ndio inakuja adhabu hiyo kwa watoto. Ikionekana adhabu imeadhibiwa watoto, maana yake shida iko kwenye ndoa. Sasa inategemea, kosa ni la wa- akina nani?  Kosa kubwa— wamama ndio wamekosea zaidi? au wababa? Kama ni wababa, ndio inakuta wanaadhibiwa, maanake inakuwa nini? Kama vile wewe ulivyojisikia raha kuingia kwa mke wa mtu, au ulijisikia vizuri, kuingia kwa mtu wa harimu wako, harimu yaani mtu ambaye hurusiwi ku- kufanya naye mapenzi. Mama yako, shangazi yako, mtu ndugu yako, dada yako— Sasa madhambi kama haya yanaleta balaa katika mji. Sasa kama wababa ndio wamekosa zaidi, mpaka watoto wakapata mlipuko wa magonjwa ule, basi wanaadhibiwa wababa. Linatokea limnyama hilo linawaingilia wanaume.
7 KATRINA; Lakini anapelekwa na: mizimu?
8 MUSTAFA; E::h na mizimu,  mizimu ndio inawapeleka. Linawaingilia wanaume. Linakwenda mpaka kipindi, ambacho lenyewe litajisikia kuacha au watu watagundua, eh? Watagundua ile tatizo, na kuanza kuenda kuiomba mizimu, “Jamani tusameheni.  Sasa tumejua makosa yetu.” Mizimu itataka kujua kama wamejua makosa lao, wataeleza kosa. Kosa ni hili,—Kama si hilo lenyewe litaendelea. Watarudia tena, kosa ni hili,— Kama silo litaendelea, mpaka lile kosa ambalo ni lenyewe,  ndio lenyewe lenyewe lenyewe mizimu itaacha.
9 KATRINA; Na Popobawa huyu ana:
10 MUSTAFA; Mh?
11 KATRINA; jina lake?
12 MUSTAFA; Huyu anaitwa Mufo. Mu fo,  Mu fo.
13 KATRINA; Maana yake ni nini?
14 MUSTAFA; Mufo ni kama mfu. Yaani aliyekufa, ni kama mizimu yaani, ni neno linalotokana na mfu. Mufo. Inaitwa Mufo au Mfu. Inaitwa Mufo. Hii ndiyo aina ya popobawa ambayo inawaadhibu wanaume. Sasa hii, haina dawa nyingine, zaidi ya kugundua kosa. Na kama hawakugundua kosa, maana sehemu nyingine, wengine wanaweza wakaamua wababa watulie. Mtu ameingiliwa na popobawa halafu akakaa kimya. Hakueleza lakini anaugua. Anaweza kumwambia mke wake tu,  “Mi naumwa.”  Lakini asieleze kinachomwumiza. Sasa mwingine si hatajua. Na mwingine akafanyiwa hivyo hivyo na yeye akaamua asiseme.  Litaendelea litawapitia litawapitia litawapitia, mpaka linaamua lenyewe linaacha.
15 KATRINA; Mm.
16 MUSTAFA; Inakuwa ni adhabu yao. M:h.
17 KATRINA; Na: kwa kawaida watu ambao wanaingiliwa na popobawa, ni Waislamu?
18 MUSTAFA; Ni:?
19 KATRINA; Waislamu? Au Wakristo wanaweza kuingiliwa pia?
20 MUSTAFA; A:h hapana, ah nanii— Hata Wakristo, lakini Waislamu wanaathirika zaidi. Kwa sababu ukanda huu wa Waislamu, ndiko zaidi kwenye mambo hayo zaidi. Kuna aina nyingi za popobawa, wanaonekana zaidi, kuliko sehemu ambazo hazina Waislamu. Kwa hiyo uwezekano wa kupata shida Waislamu zaidi, ni mkubwa zaidi. Ni mkubwa zaidi. Kuliko Wakristo. E:h. Kwa sababu eneo la- wanalo- Unajua huku kwetu Afrika mashariki, upande wa bahari ndio kwenye Waislamu.
21 KATRINA; Ndiyo.
22 MUSTAFA; Na huku ndiyo kwenye shida ya popobawa kuliko maeneo mengine.
23 KATRINA; M:h.
24 MUSTAFA; Yes.M:h.
25 KATRINA; Umetumia maneno: mbalimbali, kama mapepo,  mashetani,  majini,— Kuna tofauti gani baina ya- baina yao?
26 MUSTAFA; M::h! Shetani, labda niseme shetani, ndiyo maana yake ni “asi”, ni yule aliyeasi. Kwa hiyo shetani anaweza kuwa pepo, au anaweza kuwa mwanadamu. Au anaweza kuwa kitu yoyote. Maanake ni ile hali ya kutokubaliana na Mungu. Ndiyo shetani. Yaani kinyume cha Mungu ni shetani. Awe mwanadamu anaweza kuwa shetani.  Awe pepo, awe jini, anaweza kuwa shetani. Maana yake anayetofautiana na mapenzi ya Mungu, huyo ni shetani. Unaposema jini, “jini” ni neno la Kiswahili, linalotokana lenye asili ya Kiarabu. Waarabu wa zamani walikuwa wanatumia neno “janna.”  “Janna.”  J A double N A Janna. “Janna” kwa Kiarabu cha zamani, ni—  Maanake kilicho fichika, kisicho onekana kwa urahisi, yaani kisicho onekana kwa macho ya binadamu haya, kwa ma- kinachoonekana kwa macho ya rohoni, au, kin- kikionekana kwa macho ya- ya- ya kibinadamu, maanake kuna- kuna tukio kubwa. Kuna jambo kubwa limetokea. Hiyo. Sasa’ Waraabu wa zamani walikuwa hawajui- hawamjui Mungu, walikuwa na miungu mingi. Walikuwa wanaabudu miungu Mingi!  Waarabu wa zamani, KAbla ya Uislamu. Sasa’ ulipokuwa ukiwaambia kuwa kuna Mungu, wanakuambia tu, “Onyesha.” Kwa sababu kulikuwa- walikuwa na miungu yao, inaonekana ni masanamu, wanakwambia huyu mungu fulani, huyu anaitwa:  labda,  labda miungu ya Waarabu, kwa mfano huyu nanii “Latta,”  huyu anaitwa Latta.  Huyu anaitwa Manattah. huyu anaitwa Al Uzah. Hiyo ndiyo miungu ya Waarabu ya zamani. Ilikuwa inaonekana kwa macho. Sasa ukisema habari za Mungu, Mungu, kuna Mungu. Wanakuambia, “Yuko wapi?” Haonekani. Wanasema, “Basi ni janna,” yaani ni kitu kisichoonekana kwa macho ya kawaida. Ikiwa na pamoja na upepo pia ni janna. Kitu kisichoonekana kwa macho ya kawaida ya nyama. Na: chochote ambacho ni imani, bila kuonekana, walikuwa wanakiita Janna. Yaani kitu kilichojificha. Kitu cha kiroho. Unaona eh?  Sasa ikaendelea hata walipopata dini sasa wakaanza kujua kuna Mungu.  Mungu mwenyewe pia walikuwa wanaita Janna. Baadaye waka fanya wakafanya marekebisho, wakaona, “M-m. “Tukisema Mungu ni janna? “lakini kuna ma- kuna maroho mengine mabaya mabaya, yaani ni janna, sasa tutatofautishaje kati ya janna Mungu na janna asiye mungu? na janna shetani? Kwa hiyo wakaita jini. Jini ni roho mchafu, asiyepatana na Mungu. Lakini neno lenyewe limetoka kwenye asili ya neno la Kiarabu, la kitu kilichojificha. Kisichoonekana. Sasa baada ya kujua kwamba kuna Mungu asiyeonekana, walipojua hilo, ndio wakaamua kulibadilisha neno, kuna jini, na kuna Mungu. Ambayo siyo janna, yeye sio jini. Ni Mungu tu. Ambaye ni roho asiyeonekana lakini ni mzuri. Ehe:. Kwa hiyo kuna malaika na ninii. Na—
27 KATRINA; Na pepo?
28 MUSTAFA; Pepo ndiyo—  Wao ni hao maroho mabaya, ni hayo hayo maroho mabaya,
29 KATRINA; Ni sawa na jini?
30 MUSTAFA; E:h ni kama jini, lakini jini ingawa ina maelezo mapana kidogo. Ni roho mchafu. Ehe:.

 

License

Icon for the Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License

Dini Afrika ya Mashariki by Katrina Daly Thompson is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License, except where otherwise noted.