Sehemu ya 2: Fursa

Utamaduni: Vyeo

Salamu ya Mtaani

Soma mazumgumo ya Edo na James hapa:

Edo: Dogo, aje?

James: Shwari kabisa. Inakuwaje?

Edo: Poa. Vipi?

James: Kama kawa.

Edo: Mzigo kama kawa?

Mazumgumzo ya Edo na James ni mfano wa salamu za mtaani. Soma makala haya kuhusu salamu za mtaani zinazotumika Zanzibar. Jifundishe salamu tofauti ya mtaani, na uwe tayari kuzitumia darasani.

Umuhimu wa Vyeo

“Ila bosi, inajilipaje sasa wakati kila siku inaniharibikia?”– But boss, how will it pay for itself when it is breaking down on me every day?

James anazumgumza na bosi wake ambaye anamiliki teksi. Hafurahi na yeye, lakini bado hatumii jina lake, anamwita “bosi.” Bosi, mkuu, mkurugenzi, mheshimiwa, mwalimu, profesa, mchungaji, sheha, na dakatari ni mifano ya vyeo (titles) vya kazi. Ukitaka kuonyesha heshima, tumia vyeo. Kutumia jina la mtu badala ya cheo chake ni kutoonyesha heshima.

 

Katika mkutano huu, wafanyakazi wote wanamwita mkurugenzi, “mheshimiwa” ili kuonyesha heshima na kutambua nafasi yake.

 

Mwekezaji anaomba kukutana na mkurugenzi kwanza, lakini baada ya kuridhika na mpango wa Frank, mwekezaji alisema, “Kama ulivyosema mheshimiwa.Frank aliitwa mheshimiwa na mwekezaji, na tendo hili linaonyesha heshima. Vilevile inatambua kwamba hawahitaji kukutana na mkurugenzi kwa sababu Frank yenyewe ana vipaji sawa.

 

Baba Janet, mwanao anaumwa nyumbani.” 

Mke wa Elias anamwita Baba Janet badala ya Elias. Pia, Elias anamwita Mama Janet badala ya kutumia jina lake. Mume na mke wa familia wataitana Mama (jina la mtoto wa kwanza) na Baba (jina la mtoto wa kwanza). Kwa hivyo mtoto wa kwanza wa Elias ni Janet. Vyeo ni muhimu katika familia na mara nyingi, na kumwita mtu kwa cheo cha familia kama kaka, mume, mke, dada, ndugu, mzee, au mama inaonyesha heshima zaidi kuliko kutumia jina lao.

License

Binadamu Copyright © 2018 by Rebecca Mandich. All Rights Reserved.