Main Body
Mnyambuliko wa kufanyia (Prepositional Extension)
Katika Kiswahili, vitenzi hubadilika mara kwa mara kulingana na namna vinavyoathiriwa na mtenda (subject). Mabadiliko ya vitenzi kutokana na athari za mtenda husababisha mfanyiko (process) wa vitenzi unaoitwa “Mnyambuliko”. Kwa hivyo kuna mnyambuliko kama vile kufanya, kufanyia, kufanyiwa na kadhalika.
Mnyambuliko wa Kufanyia (Prepositional extensions)
Huonyesha kufanyika kwa kitendo “kwa niaba ya” (on behalf of). Kiambishi tamati ‘a’ kwenye kitenzi hudondoshwa (dropped) na nafasi yake kuchukuliwa (replaced with) na viambishi -ia, -ea, -lea na -lia kulingana na aina ya mzizi wa kitenzi. (the extensions -ia, -ea, -lea and -lia are determined by the root- structure of the verb which we will introduce in the next section )
Mifano:
Fanya Fanyia (Prepositional) Fanyiwa
i. Pika (cook) Pikia Pikiwa
ii. Soma (read) Somea Somewa
iii.Jenga (build) Jengea Jengewa
iv. Sema (talk/say) Semea Semewa
v. Andika (write) Andikia Andikiwa
Exercises
Study the following images. Make any three sentences using verbs in prepositional extension forms given above (Mnyambuliko wa Kufanyia). Example:
- mwalimu alitusomea hadithi
Pupils in class
A girl writing a letter to a friend
A construction worker