Main Body

Onyesho la Kwanza: Muhtasari

Ni katika Kijiji cha Patata. Kijiji kilichostawi kwa maendeleo makubwa, watu wake wakaongezeka na kuishi kwa raha na furaha. Hali hii inasababisha vijiji jirani kuitamani Patata. Lakini pamoja na haya, wanaume wanaanza kuwanyanyasa na kuwadharau wanawake. Wanawaachia kazi ya kulea watoto na kufanya kazi za nyumbani peke yao. Hali hii inafanya maendeleo ya Patata kurudi nyuma. Wahenga wa Patata hawafurahi na jambo hili. Kwa hivyo wanaamua kuleta Nguzo Mama ili kusuluhisha matatizo ya Patata. Lakini Nguzo Mama inahitaji kusimamishwa ndipo ilete maendeleo kwa Wapatata wote. Kazi ya kusimamisha Nguzo Mama ilihitaji ushirikiano wa wanawake na wanaume. Lakini wanaume wanapoona imeandikwa ‘Nguzo Mama’ wanakataa kushirikiana na wanawake kuisimamisha. Wanawake wanaachiwa wenyewe, kama walivyozoea kuachiwa kazi nyingine za nyumbani. Msimulizi anasema wanawake walifanya kazi masaa kumi na sita kwa siku. Tunaonyeshwa wanawake wenye tabia tofauti tofauti, kama vile wakulima kutoka bara, walimu, matajiri na wapenda anasa, tamaduni za kipwani, waganga wa kienyeji na makahaba. Kila mwanamke anafika peke yake, muonekano na miondoko yake ikidhihirisha hali ya maisha yake. Vilevile, maneno wanayotumia kuisifu Nguzo Mama yanaonyesha mazingira wanamotoka. Hata hivyo, kila anayejaribu kuiinua Nguzo Mama anashindwa na kuondoka jukwaani. Nguzo Mama inabaki imelala chini bila kusimamishwa.

Exercises

 

License

Materials for Swahili Learners Copyright © by kdthomp3. All Rights Reserved.