Mavazi na Majira

Utangulizi

Proficiency Level: Intermediate Low

Katika somo hili, tunajifunza kuhusu mavazi na hali ya anga (pia hali ya hewa). Kwa kawaida, mavazi huendana na hali ya anga au msimu . Kwa hivyo, unapojitayarisha kuendeleza shughuli zako za siku, ni vyema kufahamu ni mavazi yapi yanaambatana na hali ya hewa ya siku hiyo.

Nchini Kenya, kuna aina tatu za majira ambazo ni; majira ya kiangazi/joto, majira ya baridi na majira ya mvua. Tukizingatia msimu wa mvua, kuna kipindi cha masika (yaani mvua nyingi) na kipindi cha vuli (yaani mvua fupi ya rasharasha).

Kuna aina tofauti za mavazi ambazo huvaliwa wakati wa kiangazi/joto, wakati wa baridi na wakati wa mvua. Sana sana, mavazi yanayovaliwa wakati wa joto ni mepesi na yanasaidia kupunguza joto mwilini. Unaweza kuvaa mavazi haya unapokwenda kuogelea, kucheza mpira au kukimbia. Yale yanayovaliwa wakati wa baridi na jua husaidia mwili kupata joto.

Grammar and vocabulary

Hali ya anga (hali ya hewa): Weather condition

Majira: Seasons

Msimu (pl. misimu): season

Rasharasha: light showers

Exercises 1

Watch the following video on different seasons in US and Tanzania and answer the following questions

  • Name two seasons mentioned in the video
  • According to the video, what is the difference between the seasons in US and Tanzania?

 

 

License

Materials for Swahili Learners Copyright © by kdthomp3. All Rights Reserved.