USAFIRI NCHINI KENYA
Utangulizi
Kwenye somo hili,tunasoma kuhusu usafiri Afrika Mashariki. Kuna aina tatu za usafiri katika Afrika Mashariki nazo ni: usafiri wa anga, usafiri wa nchi kavu na usafiri wa maji. Kwenye usafiri wa nchi kavu, kunayo usafiri wa reli na usafiri wa barabara. Nchini Kenya, usafiri wa barabara ni maarufu sana na inaunganisha takriban kila sehemu za nchi. Matatu na teksi zinatumika sana kama vyombo vya usafiri nchini Kenya. Matatu hizi zinasimamiwa na watu na kampuni za kibinafsi. Utamaduni wa matatu ambayo inajulikana maarufu kama ‘matatu culture’ imewawezesha wamiliki wa matatu kusambaza jumbe za mapenzi kwa magwiji wa soka, riadha, pop na kadhalika. Matatu hizi zimerembeshwa na picha za watu hao maarufu. Muziki unaochezwa kwa viwango vya juu ni kawaida kwa matatu haya. Hata hivyo, kuna malalamishi kadha kuhusu tabia hii. Tazama video hii inayoonuesha tamaduni hii.
Exercises
- Write all the new vocabularies in this video
- Think about public transport in your country, how can you compare to the one in the video? Record an audio of yourself talking about this comparison.