Tamthilia hii inaitwa Nguzo Mama. Ujumbe muhimu wa tamthilia unahusu suala la maendeleo ya wanawake katika  jamii za Afrika Mashariki. Mwandishi anaonyesha harakati za wanawake katika kujikomboa kutokana na unyanyasaji na utegemezi kwa wanaume. Katika harakati hizi, wanaume wanakataa kuwaunga mkono wanawake. Vilevile, kutokana na hali ya unyanyaswaji wa muda mrefu na umaskini, wanawake wanashindwa kujiendeleza. Lakini  mwandishi anaonyesha kuwa tatizo kubwa katika harakati za kumkomboa mwanamke ni ukosefu wa umoja na upendo miongoni mwa wanawake wenyewe. Tamthilia imegawanywa katika maonyesho manne.

Tamthilia hii inatumiwa kufundishia wanafunzi wa mwaka tatu. Wanafunzi wanatakiwa kuisoma tamthilia kwa ukamilifu na kisha kutumia kazi zilizowekwa hapa kama mazoezi ya kuichambua na kuielewa tamthilia vizuri. Tunatoa muhtasari wa kila onyesho kisha mazoezi yanayohusu muhtasari huo. Pia kuna mazoezi ya msamiati na sarufi ambayo mwanafunzi anatakiwa kuyafanya kabla ya kuja darasani. Mazoezi mengine yanamhitaji mwanafunzi kuandika sentensi zaidi ya moja ili kupima uwezo wake wa kujieleza katika lugha fasaha. Pia tumeweka picha na video zinazotusaidia kuelewa zaidi tamthilia. Mwanafunzi sharti atazame video na picha kisha kufanya mazoezi yanayohusiana nazo. Maelezo mengine kwa wanafunzi yatolewe na mwalimu kama inavyohitajika.

License

Materials for Swahili Learners Copyright © by kdthomp3. All Rights Reserved.