Sura ya kwanza [1]
1 Muhtasari na mazoezi – Sura ya kwanza
Muhtasari – Sura ya kwanza
Huko kisiwa cha Ukerewe kulikuwa na mwanamke mmoja aliyeitwa Regina. Regina na jamaa yake waliishi pamoja katika kijiji cha Namagondo. Regina alikuwa mzuri sana lakini alikuwa na mume aliyemtesa. Regina alikuwa na binti watano; Rosa Mistika, Flora, Honorata, Stella, na Sperantia. Mume wa Regina aliitwa Zakaria na alitaka sana kupata mtoto wa kiume. Regina alikuwa na mimba sasa na alimwomba Mungu ampe mtoto wa kiume.
Audio Player
Usiku mmoja, Regina alikuwa akila chakula cha jioni pamoja na watoto wake. Alizungumza nao juu ya mambo ya malezi. Baadaye walikwenda kulala. Wakati huo huo, Zakaria alikuwa akirudi kutoka mahali pa kunywa pombe. Alilewa sana na alimwambia Regina kwamba alitaka kuwaona watoto wake. Watoto waliitwa isipokuwa Rosa kwa sababu Rosa alikuwa ameanza kuwa mtu mzima. Zakaria aliwaambia waimbe na kufanya mazoezi ya kijeshi. Mara Stella alimwambia baba yake kwamba Rosa alipokea barua pamoja na pesa. Zakaria alikasirika. Hakutaka binti zake watembee na mvulana ye yote. Rosa aliitwa na Zakaria na aliulizwa juu ya barua hiyo.
Audio Player
Rosa hakumtaka babake asome barua yake. Alijaribu kuila, lakini Zakaria alimshika Rosa shingo. Zakaria aliipata barua, akaisoma. Barua ilizungumzia mapenzi na Zakaria alikasirika zaidi. Alikwenda pamoja na Rosa nyumbani kwa mvulana aliyemwandikia Rosa barua. Mvulana huyo, aliitwa Charles. Zakaria alimtupia Charles shilingi, akamwambia kwamba hakutaka kumwona tena pamoja na binti yake.
Audio Player
Zoezi la 1: Kweli au Uwongo?
Answer the following true/false questions about the first chapter of Rosa Mistika.
Zoezi la 2: Maswali
Prepare the following discussion questions after reading Chapter 1 of Rosa Mistika.
Answer questions 1-9 using 1-2 complete sentences.
Question 10 requires at least 5 complete sentences.
On the final page, you will be allowed to export and save your answers as a pdf. You must save and submit your answers separately. They will not be saved here.
Regina alikuwa na shida gani nyumbani?
Regina na Zakaria wana watoto wangapi? Eleza tabia ya kila mtoto.
Regina alikuwa akifikiri juu ya nini wakati aliposikia sauti kwa mbali? Sauti hii ni ya nani?
Kwa sababu gani Zakaria hakuwepo nyumbani usiku ule?
Wakati Zakaria aliporudi nyumbani, alimtaka Regina awaamshe watoto. Kwa nini?
Stella alimwambia baba yake nini juu ya Rosa?
Rosa alijaribu kufanya nini na barua yake?
Zakaria aliona hasira nyingi wakati alipoisoma barua ya Rosa. Kwa nini alikasirika sana?
Baada ya kusoma barua ya Rosa, Zakaria na Rosa walikwenda wapi na walifanya nini?
10. Sura hii inaonyesha matatizo fulani yaliyopo katika jamii za Afrika ya Mashariki. Yajadili matatizo hayo.
On this page you will export your responses.
Feedback/Errata