Sura ya nane [8]

52 Muhtasari: Sura ya nane


Morogoro T.T.C. ilikuwa shule yenye majengo mazuri sana wakati Rosa alipoingia. Wanafunzi walikuwa wachache. Wasichana walikuwa wachache zaidi. Rosa alipofika hakuwa na nia tena ya kutafuta mchumba. Sasa alipenda kupendeza kila mvulana. Alijulikana kwa kila mvulana. Rosa alipopata mimba, alijaribu kuitoa. Alilazwa hospitali. Alipotoka aliendelea na ‘mchezo’ wake tena. Wavulana walimwita “Lab”.

Mama yake alipopata habari  kwamba Rosa alijifungua mtoto wa kiume, alimwandikia Rosa kwa furaha. Kumbe, haikuwa kweli. Rosa alipata barua nyingine kutoka Flora. Flora naye alikuwa amekwisha toa mimba.

Rosa sasa alikuwa amejulikana Morogoro nzima. Mwishowe sifa yake iliwafikia mapadri wa pale. Padri mmoja alitumwa aende kumwonyesha mwanga wa wokovu. Alipokuja aliona kitabu cha Rosa kilichoeleza habari za mapenzi, vidonge vya kuzuia mimba, furaha ya mwili, na kadhalika. Padri akaanza kuhubiri akisema, “Nimekuletea habari njema, Rosa.” Alianza kumsomea Rosa sehemu ya Biblia inayozungumzia mwanamke asherati. Alimwambia, “Rosa, wokovu uko bado machoni mwako!” Lo! Rosa alikasirika sana. Alisema kwamba maisha yake yalikuwa yamekwisha haribika, akamfukuzaPadri.

Rosa hakujali kabisa.  Aliendelea tu na maisha yake ya umalaya.

Maswali

 

License

Icon for the Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License

Mazoezi ya Rosa Mistika Copyright © by Magdalena Hauner is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License, except where otherwise noted.

Share This Book

Feedback/Errata

Comments are closed.