Sura ya sita [6]

37 Muhtasari na mchezo- Sura ya sita

Muhtasari


Rosa pamoja na wasichana wenzake walikwenda kwa basi mjini Mwanza. Walikwenda kucheza dansi na wavulana kutoka shule nyingine. Lakini kulikuwa na watu wengine humo ndani ambao walikuwa si watoto wa shule. Wao pia walicheza. Rosa alikuwa anacheza na mtu mmoja aliyeonekana kuwa mzee kidogo. Rosa alitetemeka. Moyo wake ulikuwa unamdunda. Dansi ilipokaribia mwisho, bwana huyo aliyeitwa Deogratias alimbusu Rosa.

Rosa aliporudi chumbani kwake alishindwa kupata usingizi. Alikwenda katika chumba cha rafiki yake Thereza, akaanza kumbusu kwa tamaa isiyopungua. Mwishowe Rosa aliona kwamba anachohitaji ni rafiki wa kiume.

Asubuhi Rosa alianza kutafuta barua alizoandikiwa na wavulana zamani. Mvulana mmoja hakumtosha. Rosa alianza mapenzi, lakini aliwachezea tu wavulana. Hakuwapenda. Alimpenda Deogratias tu, akifikiri kwamba Deogratias ndiye atamwoa.

Sista John alivumbua kwamba Rosa alianza kulala mjini. Siku moja alimwita ofisini na kumwambia kwamba atapelekwa nyumbani. “Utarudi tu kufanya mtihani wako wa ‘Cambridge'”, Sista John alisema.

Rosa alikwenda nyumbani. Aliwaambia wazazi wake kwamba akili zilimzidi kichwani, lakini wazazi walivumbua ukweli. Walisikitika. Zakaria aliendelea kuwachunga binti zake zaidi. Emmanuel alitunzwa vizuri sana.

Alipokuwa akikaa nyumbani Ukerewe, Rosa alipata barua ndefu sana kutoka kwa Deogratias. Alipoisoma alifurahi sana: Deogratias alisema atamwoa wakati wo wote. Rosa aliibusu barua hiyo. Chumba chake kilikuwa kimejaa picha za Deogratias.

Mtihani ulipofika, Rosa alishinda masomo matatu tu, lakini hata hivyo alichaguliwa kwenda Morogoro T.T.C. Alifurahi.

Mchezo

Exercises

 

License

Icon for the Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License

Mazoezi ya Rosa Mistika Copyright © by Magdalena Hauner is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License, except where otherwise noted.

Share This Book

Feedback/Errata

Comments are closed.