Madhumuni kuu ya kozi hii ni kuwasaidia kufahamu riwaya hii maarufu ya Rosa Mistika. Baada ya kusoma Kiswahili kwa mwaka mmoja tu si rahisi hata kidogo kuanza kusoma kilichokusudiwa kusomwa na wananchi wa Afrika ya Mashariki. Lakini kuna mengi ya maana katika kitabu hicho, yanayotusaidia kuelewa maisha ya watu wa huko.

Katika sehemu ya Kamusi hamtapata maneno yote yanayowashinda, bali baadhi yao tu, kwa hiyo itawabidi kutumia kamusi nyingine ya Kiswahili-Kiingereza.

Sehemu ya Maswali ina madhumuni matatu, nayo ni (1) kuhakikisha kwamba mmeelewa yaliyomo, (2) kuwawezesha kuzungumza juu ya yaliyomo kwa njia rahisi-ndiyo maana kuna maswali rahisi kama, ‘Regina na Zakaria wana watoto wangapi?’, na (3) kuzungumza juu ya maswala makuu ya kijamii na kisiasa. Mara nyingine ni vigumu sana kwa wanafunzi kujadili maswala haya kwa Kiswahili, hasa kwenye mwanzo wa muhula. Hapo kutumia Kiingereza si dhambi.

Sehemu za Sarufi zinatumia sana msamiati wa sura inayohusika, kwa hiyo ni muhimu sana kukariri msamiati wake wote.

Michezo inafurahisha na kuwawezesha wanafunzi kuongea. Na kuongea kwa Kiswahili ndiyo madhumuni mengine kubwa ya kozi hii. Wanafunzi, saidieni kwa kutunga michezo mipya.

Hatimaye, kozi hii inaonyesha jamii ya Tanzania kuanzia miaka ya sitini mpaka siku hizi. Inaonyesha hali halisi, siyo hali ambayo mwandishi angependa iwepo.

License

Icon for the Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License

Mazoezi ya Rosa Mistika by Magdalena Hauner is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License, except where otherwise noted.

Share This Book

Feedback/Errata

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *