Sura ya kumi [10]

68 Muhtasari na Maswali: Sura ya kumi

Muhtasari


Kameya, Rosa hakukaa zaidi ya majuma mawili kabla ya kurudi Morogoro. Alikwenda kumaliza kipindi cha mwisho. Rosa alijiona mwalimu.

Boti ilichukua saa tatu kutoka Nansio mpaka Mwanza. Botini Rosa aliona mtoto mdogo. Mtoto alimpenda sana Rosa, hata akalala mikononi mwake. Rosa alitamani sana kupata mtoto.

Mjini Mwanza Rosa alimtembelea dada yake Flora katika shule ya ‘Jela’. Flora alinung’unika sana, eti wote wanalindwa kama watoto wadogo, lakini hata hivyo hupata mimba. Dada hao walikumbuka jinsi Zakaria alivyowalinda. Rosa alipoondoka shule ya ‘Jela’, alikwenda kwa basi mpaka Mwanza. Humo basini alisikia kijana mmoja akizungumza na rafiki yake; “Wasichana wa shule hii wanalindwa! Wanapoteza uwezo wao wa kuchagua!”

Rosa alisafiri mpaka Morogoro. Alikwenda moja kwa moja kumwona mkuu wa chuo, lakini kumbe alikuwa hayupo. Badala yake alimkuta Mwalimu Albert. Mwalimu Albert, kwa vile alisikia sifa mbaya ya Rosa, alimfukuza. Rosa aliporudi chumbani mwake, alijaribu kujiua kwa kisu. Hata hivyo, alipopona, alipelekwa nyumbani. Baada ya siku moja tu lakini Rosa alirudi, akamwomba Mwalimu Albert ampe nafasi ya mwisho ajirekebishe.

Rosa karibu alishindwa na mitihani ya mwisho, lakini mwishowe alishinda. Pendekezo lake lilikuwa kufundisha katika mkoa wa Mwanza, karibu na Ukerewe. Alipata kazi katika shule ya msingi Nyakabungo huko huko Mwanza. Huko, Rosa alitaka kuanza kuishi maisha.

 

Maswali

 

License

Icon for the Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License

Mazoezi ya Rosa Mistika Copyright © by Magdalena Hauner is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License, except where otherwise noted.

Share This Book

Feedback/Errata

Comments are closed.