Sura ya saba [7]

44 Muhtasari na Mchezo- Sura ya saba

Muhtasari


Kina Zakaria walimngoja sana mgeni wao. Walifurahi sana waliposikia kwamba mchumba wa Rosa, Deogratias, atawatembelea. Alipofika, alikaribishwa vizuri sana. Kila siku kuku mmoja alichinjwa, na Deogratias alipewa muda mrefu wa kuzungumza na mchumba wake. Zakaria alimweleza mahitaji yake katika swala la mahari. Alitaka Deogratias atoe ng’ombe wanne, mbuzi wawili, kinu, viti vitatu, na shilingi elfu moja. Pia, Zakaria alimwambia Deogratias kwamba atamtuma kwa jamaa wote na kwa jamaa wa Regina pia, “maana mtoto si wangu peke yangu.” Deogratias alikubali hayo yote.

Siku moja Zakaria alimpeleka Deogratias kunywa pombe ya moshi. Walikunywa mpaka usiku. Mara, watu walianza kukimbia ovyo: mahali penyewe palizungukwa na polisi. Zakaria alikimbia, lakini mgeni wake alishikwa, akatembea kwa miguu mpaka gerezani. Deogratias alihukumiwa kufungwa miaka miwili kwa kunywa pombe ya moshi.

Rosa alifunga safari kwenda Morogoro. Njiani alisikia wanawake wawili wakizungumza juu ya Deogratias. Alisikia kwamba alikuwa ameoa wake wawili, na kwamba anawachezea watoto wa shule. Alishangaa kweli aliposikia habari za mchumba wake – Bwana Maendeleo mjini Mwanza. Alichoma barua na picha zake zote.

Rosa alitaka kujifurahisha kidogo, ili amsahau Deogratias. Aliingia katika baa moja mjini Mwanza, akaanza kunywa na kusikiliza mazungumzo ya wanaume na wanawake. Kweli ameyasikia mengi, hasa juu ya wanawake kuwanyonya wanaume. Alisikia wanawake wawili wakiwaambia wanaume wawili, “Njooni kesho mtuchukue. Sisi ni mali yenu tu!” Kwa kweli wanawake hao walidanganya tu, wakitaka kula pesa za watu.

Hata Rosa naye alianzisha “mapenzi” ya namna hiyo.

mchezo

Maswali

 

License

Icon for the Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License

Mazoezi ya Rosa Mistika Copyright © by Magdalena Hauner is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License, except where otherwise noted.

Share This Book

Feedback/Errata

Comments are closed.