Sura ya kumi na moja [11]
80 Matumizi ya Lugha
SARUFI:
(1) VIUNGO/VIUNGANISHI
(2) VIHISISHI
VIUNGO/Viunganishi/Conjunctions
A conjunction is a part of speech that connects words, phrases, clauses or even sentences.
Examples: a) Hannah anasoma. Hannah anasikiza muziki. Join the two sentences – Hannah anasoma hali anasikiza muziki/ Hannah anasoma huku akisikiza muziki. Hannah is reading as she listens to music/Hannah is reading while listening to music.
b) Daudi atakuja tu. Amechelewa. Ingawa Daudi amechelewa, atakuja tu. Although Daudi is late, he will still come.
c) Amiin ni Muislamu. Hali chakula kwa sababu amefunga. Amiin ni Muislamu, ndio maana hali chakula kwa sababu amefunga. Amiin is Muslim, that’s why he is not eating because he is fasting.
hali while, as, -ing
huku while, as, -ing
ili so that, in order that
ingawa although
isipokuwa except, … that, …for
kama kwamba as if, as though
ndiyo maana that’s why
ndiyo sababu that’s why
wakati when, while
yaani that is, that’s to say, i.e.
Zoezi la kwanza
TAFSIRI. JAZA PENGO. TRANSLATE. FILL IN THE CORRECT CONJUNCTION.
- Regina alikuwa mwanamke mwenye busara hakuwa na kisomo cho chote (12).
- Nyoka alionekana alikuwa amebanwa na mlango (13).
- “Kumbe uko mnyamavu namna hii! Ulifikiri tutafukuzwa!” (28)
- Nywele nyeupe – hazikuwa nyingi – ziliweza kuonekana (40).
- Rosa alikwenda chumbani mwake akilia (65).
- Albert alikuwa akifanya kazi akipika chakula cha jioni (67).
- Mtu wa shamba huangalia nyota apate kulima zao fulani (71).
- “Sura yako naikumbuka jina nimesahau.” (74)
- Aliona ni yule Charles wa zamani, ndevu (76).
Vihisishi/interjection
aa! oh no, hold on there (disagreement)
a! a! a! oh no! oh my god!
hebu c’mon, let’s …..
kumbe lo and behold, bingo! surprise!
lo; loo wow, surprise, amazement, fear
ooo! oh; I see
ooo? is that so?
Hewaa/ewaa! accent, agreement with proposition
Do!/Du! – surprise
Zoezi la pili
TAFSIRI NA JAZA. TRANSLATE AND FILL IN THE CORRECT INTERJECTION.
1 Alikwenda kuzima koroboi. ………..! Aliona nyoka mkubwa mweusi
[….]. (12)
2 “Mimi fikiri wewe iko fanya kaji majuri (= unafanya kazi vizuri), ……….
danganya.” Baniani alifoka. (15)
3 Ilikuwa mara ya kwanza kwa Stella kuona walevi – […] “Angalia!
Angalia! ….. ….. …..!” (19)
4 “Mnataka nini watoto wangu?”
“Mzee sisi tunatafuta mayai ya kununua.”
“ …….! ……….. mnatafuta mayai tu.” Ninayo machache. [….] (23)
5 “Zakaria, inafaa uache ulevi.”
“ ……….. mke wangu, unafikiri ulevi ni ugonjwa?” (24)
6 “Flora, …….. tuone picha za boys wako!” (63)
Zoezi la tatu. MCHEZO MFUPI.
Wanafunzi waandae michezo mifupi kwenye vikundi, wakitumia mifano mingi ya
tanakali sauti.
Feedback/Errata