Sura ya kumi [10]
72 Matumizi ya Lugha
Sarufi: Kirejeshi Kisicho Tensi
The tenseless relative construction refers to actions taking place in the general or ‘universal’ present, i.e. the present expressed by the tenses -a- and hu-. It is often used in proverbs.
- kisiwa kijulikanacho
- known island/island that’s known (3)
- mtu awezaye kuendesha shule vizuri (80)
- someone able to (who can) run a school well
- kazi wafanyazo
- activities (which) they do (57)
- mwezi ujao
- month which is coming/next month
- swali lifuatalo
- the following question
- kisiwa kisichojulikana
- unknown island/island which isn’t known
- mtu asiyeweza …
- someone unable/who can’t…
- kazi wasizofanya
- activities (which) they don’t do
- mwezi usiokuja
- month which isn’t coming
-
swali lisilofuata
the question which doesn’t follow
Methali:
- Ajuaye ni Mungu.
The one who knows is God. (Only God has true knowledge.)Mtoto umleavyo ndiyo akuavyo.
How you raise a child, that’s how s/he’ll grow.
Zoezi la kwanza. BADILISHA TENSI.
Tafsiri sentensi zifuatazo. Badilisha tensi na kutumia sarufi mpya, yaani Virejeshi Visivyo Tensi.
1 Mtu anayesoma madarasa mengi ni msomi.
2 Simba anayejulikana si mkali.
3 Lugha zinazofundishwa kwa kawaida ni Kixhosa na Kikikuyu.
4 Watu wanaoandika riwaya ni waandishi.
5 Dini inayotawala Unguja ni Islam.
6 Juma linalokuja litakuwa refu.
7 Wiki inayokuja haitakuwa rahisi.
Zoezi la pili. TAFSIRI METHALI.
1 Kila apigaye (hodi) mlango hupata majibu.
2 Yote yang’aayo usidhani ni dhahabu. (ng’aa=shine, glitter)
3 Kikulacho ki nguoni mwako. (ki=kimo)
4 Asiyeuliza hanalo ajifunzalo.
5 Amnyimaye punda adesi, kampunguzia mashuzi. (nyima=deny, adesi
9/10=lentil, shuzi 5/6=fart)
6 Aisifuye mvua, imemnyea. (sifu = praise, nya = excrete; rain)
Zoezi la tatu. MAELEZO YA METHALI.
Andika insha inayoeleza maana ya methali moja. Utapata methali nyingi kwenye mtandao:
http://www.glcom.com/hassan/kanga.html.
http://web.ionsys.com/~mourad/methali.htm
Kanga Gallery
http://www.swahilionline.com/language/proverbs/provrbs.htm
Feedback/Errata