"

Sura ya kwanza [1]

8 Matumizi ya Lugha

Zoezi la kwanza: Marudio ya Ngeli

Tunga mazungumzo mafupi ukitimua maneno yafuatayo.  Tunga sentensi kama unavyoonyeshwa katika mfano.
[Create a short conversation using each of the nouns below as the subject of a sentence, following the example.]

MFANO
A:            Kitu kimoja kilimsaidia Regina.
B:            Kitu gani?
A:            Ng’ombe.

PATTERN:
A: One thing helped Regina.
B: What thing?
A: Cattle/cows.

1            kijiji
2            mwanamke
3            kijana
4            ng’ombe
5            barua
6            shamba
7            Tumia maneno yako.

Zoezi la pili: Marudio ya Tensi: Kanusha Wakati Uliopo  
Badilisha sentensi kama unavyoonyeshwa hapa chini.
[Review of the tenses. Negate the present tense. Change the sentences as shown below.]

MFANO

A            Je, Regina anakaa Dar es Salaam?
B            Hapana, (Regina) hakai Dar es Salaam.

1          Je, tunasema Kichina hapa?                                                             
2          Je, unafahamu kila kitu?
3          Je, mnafanya kazi kwa bidii?
4          Je, wanafunzi wanajibu?
5          Je, Ukerewe unajulikana?
6          Je, miaka inapita?
7          Je, upepo unavuma?
8          Je, kazi inatosha?
9          Je, majirani wanasema?

Zoezi la tatu: Kanusha katika Wakati Uliopita na Wakati Ujao 
Tumia sentensi zilizopo katika Zoezi la pili.
[Negate in the past tense and the future tense. Use the sentences from Exercise 2 (change them to future and past tense).]

Zoezi la nne: Vimilikishi  (Binadamu na vimilikishi vyake.)
Jaza nafasi.
[Possessives. (Human beings and their possessives.) Fill in the blanks.]

1          baba    _ake
2          mama   _angu
3          mume _ake
4          dada   _ako
5          mgeni   _enu
6          binti   _ao
7          mwanafunzi   _etu
8          kiongozi   _etu
9          Tumia nomino yoyote utakayochagua (Use a noun of your choice).

Zoezi la tano: Virejeshi
Tunga sentensi kama unavyoonyeshwa katika mfano.
[The Relatives. Form sentences as (you are) shown in the pattern.]

MFANO

A          Sitaki nyama iLIyooza.
B          Bila shaka. Tuna nyama nzuri iSIyooza.

1          chakula
2          mkate
3          maziwa
4          nyanya
5          embe
6          yai
7          samaki
8        Tumia nomino yoyote utakayochagua (Use a noun of your choice).

Zoezi la sita: Virejeshi
Tafsiri. [The Relatives.   Translate.]

1          The girl who was known as Rosa Mistika was fifteen.
2          The author who wrote Rosa Mistika comes from Nansio.
3          Kikerewe is a language which is spoken in Ukerewe.
4          The father wasn’t someone known as a good teacher. […wasn’t a person who
was known as…]
5          Andika sentensi yako.

Zoezi la saba: Mazumgumzo
Mwanzo wa muhula: mazungumzo baada ya likizo.
Ongea na wanafunzi wenzako kwa dakika 5 – 10, kisha mweleze mwalimu habari hizo.

1.          Ulikaa wapi wakati wa likizo?
2.         Ulifanya nini?
3.         Ulikuwa na afya nzuri? Uliumwa?
4.         Ulifurahi zaidi kufanya nini?
5.         Uko tayari kusoma tena?
6.         Umesahau Kiswahili sana?
7          Umeshanunua vitabu vyote?
8.         Je, utahudhuria meza ya Kiswahili?
9.         Je, unaweza kumsaidia mwanafunzi wa mwaka wa kwanza?
10.       Karibu uulize maswali yako wewe (Use any other questions).

License

Icon for the Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License

Mazoezi ya Rosa Mistika Copyright © by Magdalena Hauner is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License, except where otherwise noted.

Share This Book

Feedback/Errata

Comments are closed.