Sura ya pili [2]
15 Matumizi ya Lugha
SARUFI: KUWA NA
Kitenzi kuwa kinatumika katika tensi mbalimbali zinazoitwa Tensi za Maneno Mawili, kama vile nilikuwa nikisema, ‘I was saying’, n.k. (=na kadhalika). Kitenzi kuwa na, ‘to have’ kinatumika zaidi.
Zoezi la kwanza. WAKATI ULIOPITA; WAKATI ULIOPO.
Badilisha sentensi kama unavyoonyeshwa katika mfano.
* Regina alikuwa na watoto watano.
–> A: Kumbe, Regina ana watoto watano?
B: Ndiyo, anao.
_______________________________________
1 Chumba kilikuwa na watoto.
2 Wachawi walikuwa na nguvu.
3 Namagondo ilikuwa na nyumba chache.
4 Samaki alikuwa na miba.
5 Mzigo ulikuwa na kufuli.
6 Honorata alikuwa na shamba la pamba.
[Pattern translated: * Regina had five children. –> A: So Regina has five children? B: Yes, she does (have them).]
Zoezi la pili. KANUSHA WAKATI ULIOPITA.
Badilisha sentensi katika Zoezi la pili kama unavyoonyeshwa katika mfano.
* Regina alikuwa na watoto watano.
–> A: Kumbe nimesikia eti hakuwa na watano.
B: Kumbe!
_________________________________________
[Pattern translated: * Regina had five children. –> A: Hm, I heard that she didn’t have five. B: Hm!]
Zoezi la tatu. KANUSHA WAKATI UJAO.
Tunga sentensi zenye sarufi hii ukitumia picha za kutoka mtandaoni, kama AfricaFocus: http://africafocus.library.wisc.edu/
atakuwa na (s/he will have)
hatakuwa na (s/he won’t have)
Feedback/Errata