"

Sura ya tatu [3]

17 Muhtasari – Sura ya tatu

3sportshop

Rosa aliangalia kalenda kila siku. Hakuweza kungoja mpaka aende shule. Siku moja alikwenda mjini Nansio kununua viatu vipya. Flora alikwenda pamoja naye.


Mjini Nansio, waliingia duka moja la Mhindi. Jirani yao Ndalo alifanya kazi humo na walifikiri kwamba angeawasaidia kununua viatu kwa bei nzuri. Lakini Mhindi hakutaka kupunguza bei, akimtukana Ndalo kwamba anaharibu biashara yake. Wasichana wakaingia duka lingine, wakapata viatu kwa bei nzuri.

Siku moja Zakaria aliondoka kwenda kunywa kama kawaida yake. Siku hiyo alilewa zaidi, hata akaletwa nyumbani akibebwa na Ndalo na mtu mwingine. Walimlaza kitandani, wakamwacha alale. Regina alifahamu kwamba Zakaria alikuwa amechukua pesa zote za Rosa, akanunua chupa nyingi za pombe. Safari ya Rosa ilivunjika. Hayo yote Regina alipata kujua alipowatembelea Ndalo na Bigeyo.

Ndalo na Bigeyo walisumbuliwa sana na taabu ya uzazi. Bigeyo alishindwa kupata mimba. Walitembea mpaka mbali kwa waganga wengi wapate mashauri, lakini – wapi! Walishindwa. Mganga mmoja aliwashauri wale nyama ya kuku wakikimbia kuzunguka nyumba.

Regina alitaka sana kumsaidia Rosa aende shule. Mwishowe, akapata wazo zuri. Alianza kupika pombe ya kienyeji inayoitwa mapuya. Ni pombe ya muhogo. Zakaria hakusema kitu. Wasichana walikuwa wakimsaidia mama yao kutayarisha kila kitu. Pombe ikawa tayari. Watu wengi walikuja katika mji wa Zakaria. Walinunua pombe nyingi wakanywa, wakicheza, na hatimaye wakifanya mambo yao ya kilevi. Watoto waliona walevi kwa mara ya kwanza katika maisha yao. Honorata alikodoa macho alipoona mtu mmoja anakojoa karibu nao.

Regina na Rosa walihesabu pesa, wakakuta. Walifurahi sana.

Sura ya 3: Kweli au Uwongo

Maswali

 

 

License

Icon for the Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License

Mazoezi ya Rosa Mistika Copyright © by Magdalena Hauner is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License, except where otherwise noted.

Share This Book

Feedback/Errata

Comments are closed.