Sura ya kumi na mbili [12]

82 Muhtasari na Mchezo: Sura ya kumi na mbili

Muhtasari


Siku moja Rosa alipofika shule, aliiona kalamu yake juu ya meza yake. Kulikuwa na barua pia. Aliisoma, akashangaa kwa sababu ilisema kwamba asipohama mtaa wa Uhuru, atakufa. Alikwenda kituo cha polisi kuonyesha barua. Rosa aliwaambia polisi jina la mtu ambaye ni adui yake. Mwanamke huyu aliitwa, akalazimishwa kuandika karatasi ili polisi waweze kujua kama ameandika barua hii. Mwandiko wake ulikuwa tofauti. Polisi walimwambia Rosa ahame. Alihamia chumba cha mchumba wake.

Charles na Rosa walikuwa wakipanga safari ya kwenda Ukerewe kuwatembelea wazazi wao. Siku moja, Flora alikuja nyumbani kwa Charles na Rosa. Walizungumza na walikula chakula pamoja. Walipomaliza kula, Charles alileta chupa ya mvinyo. Charles na Flora walikunywa kiasi, lakini Rosa alikunywa sana. Baadaye, Charles alimsindikiza Flora hadi kituo cha basi.

Charles aliporudi nyumbani, alimwona Rosa katika hali mbaya kidogo. Alikuwa amelala kitandani mguu mmoja ametupa huku na mwingine huko. Charles alimlaza vizuri na kumfunika. Alianza kusoma. Baada ya muda alipata tamaa mbaya. Alianza kufikiri juu ya maneno ya kijana aliyezungumza juu ya Rosa. “Lazima uwe macho. Wanawake wengine wanatembeatembea ovyo; siku ya kuolewa bwana zao wanasema walikuwa mabikira. Wanawake kama hao hutumia dawa……” Charles alifikiri kwamba Rosa alikuwa amelala fofofo. Hakudhani kwamba Rosa ataweza kujitambua kesho. Alijaribu kumwamsha. Alimshika Rosa na kusema “Rosa! Amka! Amka!” Rosa hakuamka. Charles alimshika tena. Aliona kwamba Rosa alipoteza fahamu yake yote.

Charles alifanya jambo baya mno. Baada ya kuvua nguo za Rosa na nguo zake, Charles alilala naye. Alifanya hivi ili aweze kujua kama alikuwa kweli bikira. Baadaye, alimsafisha Rosa vizuri sana ili asije akatambua yaliyotokea usiku ule.

Asubuhi, Rosa alikuwa wa kwanza kuamka. Alimwamsha Charles na kumwambia kwamba hakuweza kukumbuka mambo yaliyotokea usiku. Charles alimwambia walikuwa wakinywa pamoja. Baadaye, wakaanza kutayarisha vitu vya kwenda navyo nyumbani.

Mchezo

Maswali

 

License

Icon for the Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License

Mazoezi ya Rosa Mistika Copyright © by Magdalena Hauner is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License, except where otherwise noted.

Share This Book

Feedback/Errata

Comments are closed.