"

Sura ya kumi na moja [11]

74 Muhtasari: Sura ya kumi na moja

 


Rosa, akiwa na matumaini ya kugeuza maisha yake, alikwenda kufundisha katika shule ya msingi Nyakabungo. Alijipatia chumba cha kupanga. Alijitunza sana. Alifanya kazi yake ya ualimu vizuri. Hakumkaribisha mwanamume ye yote ndani ya chumba chake.

Sifa yake ilivuma sana mjini. Mwishowe ilimfikia mvulana aliyekuwa akifundisha shule ya msingi ya Kirumba, humo humo mjini. Mwalimu huyo alikuwa mgeni pia huko Mwanza. Kwa muda mrefu mwalimu huyu alikuwa ametafuta mwanamke msichana wa kuoa. Wasichana wote aliokuwa nao zamani aliwakataa kwa sababu walitembeatembea na vijana wengine. Aliposikia sifa ya Rosa aliulizauliza nambari ya chumba chake na barabara, hata mwishowe akakifahamu.

Siku moja mwalimu huyu alikuja mpaka chumbani kwa Rosa, akampa barua, akaondoka. Rosa mara tu alipomwona alianza kumpenda. Aliifungua barua, akaangalia jina la mwandishi. Aliona ni Charles Lusato. Barua yenyewe ilikuwa ya mapenzi Rosa alifikiri, “Kijana huyu lazima anioe, nikimkataa huyu, basi maisha yangu yamekwisha, sina tumaini tena.”

Rosa alianza tena maisha ya mahaba. Charles pia alimpenda sana Rosa. Walikwenda kwenye dansi pamoja, au sinema. Rosa alimtembelea Charles mara nyingi. Nyumbani walizoea kubusiana. Siku moja walipokuwa wakibusiana, Charles alimwangusha Rosa juu ya kitanda. Mara Rosa alimwomba asimharibu kabla ya muda, angoje mpaka siku watakayooana. Alimwambia, “Charles, mimi ni bikira.” Charles akampa heshima yake yote aliposikia maneno hayo.

Kwa bahati mbaya rafiki wawili wa Charles walishangaa sana walipoambiwa naye kwamba mchumba wake ni bikira. Wakamweleza hadithi yote ya Rosa. Lakini Charles aliendelea kumheshimu Rosa. Alivumilia maneno ya watu. Alikuwa amekwisha kata shauri kumwoa Rosa – bikira. Charles katika maisha yake aliwaomba uchumba wasichana siku ya kwanza kuonana nao.

Wachumba hawa walianza kufanya mpango wa arusi. Walianza kupanga safari ya kwenda nyumbani kwa wazee wao.

Maswali

 

 

License

Icon for the Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License

Mazoezi ya Rosa Mistika Copyright © by Magdalena Hauner is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License, except where otherwise noted.

Share This Book

Feedback/Errata

Comments are closed.