"

Sura ya nne [4]

24 Muhtasari – Sura ya nne na Maswali

Muhtasari


Rosa alikwenda shule ya wasichana ya Rosary, karibu na mji wa Mwanza. Shule hii ilikuwa karibu na shule nyingine za wavulana, kwa hiyo kila msichana alikuwa na rafiki wa kiume.

Shule hii ilikuwa ikiendeshwa na mabikira. Wasichana waliwaita masista. Mkuu wa shule aliitwa Sista John.

Rosa alikuwa bado hataki kuzungumza na mvulana ye yote. Wavulana wengi walimletea barua, lakini yeye alijibu tu, “Samahani kaka, jaribu mahali pengine.” Masista walimwita Rosa msichana mwema na mwenye bidii. Sista John alimchagua kuwa mkubwa wa darasa lake. Wasichana wote pia walimpenda.

Baada ya kipindi cha kwanza Rosa alirudi nyumbani Ukerewe. Alinenepa na watu walikuwa wakimwambia kwamba alikuwa mzuri zaidi. Siku moja Rosa aliitwa na mama yake. Aliambiwa aende kumwita Bigeyo. Rosa alimweleza Bigeyo ugonjwa wa mama yake. Bigeyo alifahamu, akakimbia kumsaidia Regina. Regina alijifungua mtoto wa kiume. Bigeyo alipiga vigelegele kwa furaha. Zakaria pia alifurahi, akampa pongezi mke wake, “Regina! Sasa mji huu umekuwa wako.” Kwa vile alifurahi sana, alikwenda mjini kununua vitu vyote walivyotaka Regina na Rosa. Lakini Zakaria hakuacha ulevi.

Siku za Rosa zilipokwisha, mtoto alikuwa ameshabatizwa kwa jina la Emmanuel. Alikuwa mtoto mwenye afya nzuri na nyumbani dada zake walimpenda.

Maswali

License

Icon for the Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License

Mazoezi ya Rosa Mistika Copyright © by Magdalena Hauner is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License, except where otherwise noted.

Share This Book

Feedback/Errata

Comments are closed.