"

Sura ya tano [5]

31 Muhtasari na Mchezo- Sura ya tano

Muhtasari


Rosa alirudi shuleni, lakini kipindi hiki hakikuwa kizuri sana, hasa kwa Rosa. Wanafunzi walianza kuzoea maisha ya shuleni. Walianza fujo ya kuzungumza darasani, walipiga kelele, na walichelewa kumaliza kazi yao. Rosa aliitwa na Sista John ofisini. Sista John alimtaka amwambie majina ya wanafunzi wanaofanya fujo. Rosa alikataa. Darasa lote likapewa adhabu ya kufyeka majani yote yaliyokuwa karibu na shule.

Mwezi uliofuata Sista John alimwita Rosa tena. Alisikia kwamba wasichana wengine walilala mjini, wakarudishwa asubuhi kwa motokaa, bado wamelewa. Rosa alikataa tena kumwambia majina, lakini Sista John alimwonya kwamba atafukuzwa shule kama hatamwambia. Rosa alitaja majina matatu.

Wale wasichana waliitwa. Walipewa adhabu ya kusonga magari mia ya mchanga. Kazi hii ilikuwa ngumu sana. Vidole vyao vilivimba. Siku moja Rosa alipofungua deski lake, aliona madaftari yake yote yalitatuliwa na shuka zake zilichomwa moto. Alilia kwa sauti, akamwambia Sista John. Wasichana wale watatu walifukuzwa shule. Walisafirishwa makwao.

Rosa alimaliza darasa hili la tisa kwa shida, lakini bado alikuwa wa nne katika mtihani wa mwisho.

Mara chache Rosa alikwenda kutembea mjini Mwanza. Siku moja alisikia wavulana wawili wakimzungumzia. Walisema kwamba Rosa hapendi kutembea na wavulana kwa sababu labda yeye ni kilema. Maneno hayo yalimsumbua sana moyoni. Alikata shauri kwenda kucheza dansi.

Exercises

 

License

Icon for the Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License

Mazoezi ya Rosa Mistika Copyright © by Magdalena Hauner is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License, except where otherwise noted.

Share This Book

Feedback/Errata

Comments are closed.