"

Utangulizi (Introduction)

Lengo kuu la kozi hii ni kuwasaidia kufahamu riwaya hii maarufu ya Rosa Mistika. Baada ya kusoma Kiswahili kwa mwaka mmoja tu, si rahisi hata kidogo kuanza kusoma na kuelewa kama wazungumzaji wa Kiswahili huko Afrika ya Mashariki. Lakini kuna mengi ya maana katika riwaya ya Rosa Mistika. Riwaya hii itatatusaidia kuelewa maisha ya watu huko Afrika Mashariki.

Katika Kamusi hamtapata maana ya maneno yote msiyoyajua , bali baadhi yao tu.  Kwa hiyo itawabidi kutumia kamusi nyingine ya Kiswahili-Kiingereza.

Sehemu ya Maswali ina malengo matatu, nayo ni: (1) kuhakikisha kwamba mmeelewa yaliyomo, (2) kuwawezesha kuzungumza juu ya yaliyomo kwa njia rahisi-ndiyo maana kuna maswali rahisi kama, ‘Regina na Zakaria wana watoto wangapi?’, na (3) kuzungumza juu ya maswala makuu ya kijamii na kisiasa. Wakati mwingine ni vigumu sana kwa wanafunzi kujadili maswala haya kwa Kiswahili, hasa mwanzoni mwa muhula. Hapo kutumia Kiingereza si dhambi.

Sehemu za Sarufi zinatumia sana msamiati wa sura inayohusika, kwa hiyo ni muhimu kukariri msamiati huu kwa makini.

Michezo inafurahisha na kuwawezesha wanafunzi kuongea. Na kuongea kwa Kiswahili ndiyo madhumuni mengine kubwa ya kozi hii. Wanafunzi, saidieni kwa kutunga michezo mipya.

Hatimaye, kozi hii inaonyesha jamii ya Tanzania kuanzia miaka ya sitini mpaka siku hizi. Inaonyesha hali halisi, siyo hali ambayo mwandishi angependa iwepo.

License

Icon for the Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License

Mazoezi ya Rosa Mistika Copyright © by Magdalena Hauner is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License, except where otherwise noted.

Share This Book

Feedback/Errata

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *