Swahili

Advanced: Unataka kujifunza kuhusu utamaduini au usomaji?

Kwa sura hii, tutajisomea kuhusu vitabu visomaji kuchunguza vipengele vya utamaduni wa Tanzania na pia kujadili historiographia ya taifa au ya pwani ya Uswahili.

Askew, Kelly Michelle. Performing the Nation: Swahili Music and Cultural Politics in Tanzania. Chicago: University of Chicago Press, 2002.

Kufanya Taifa: Muziki ya Uswahili na Siasa za Utamaduni Nchini Tanzania, na Kelly M. Askew kinachambua historia na maana ya kitamduni ya muziki ya taarab, dansi, na ngoma. Askew anawasilisha muktadha wa kihistoria kuonyesha jinsi ya tamaduni hizi zilivyotokea kwa miaka tisini. Ngoma ndio aina ya zamani zaidi ya maonyesho mengine, na kila moja inawakilisha unshawishi wa anga tofauti kwa jamii ya Uswahli–ya wenyeji, kitafi, na ya dunia. Askew anadai kwamba maonyesho haya yalikuwa ushawishi mkubwa kwa maendeleo ya kitaifa. Lakini kuna nguvu katika mahali ambapo watu wanacheza muziki na dansi. Cha kupendeza, Askew anathibitisha si kuhusu wanguvi kujenga taifa, badala yake ni mjadala kati ya wanasiasa na maraia. Anaonyesha kuna safu za nguvu kwenye maonyesho haya ya densi. Kwa mfano, watu wantatua maswala au kudai mamlaka. Katika maonyesho hata ya taarab ambapo watazamaji mara nyingi huwa Waislamu, wanwake wanadai nguvi, wakitumia nafasi kama nafasi ya kucheza muziki, kuonyesha na kujadili maswala yanayohusiana na maeno. Kwa kiwango chini au juu ambapo watu wanaeleza kama wanakubali wa watu wanguvi au hapana, Askew anaonyesha nafasi ambapo kuna mjadala ya mwili badaala ya sauti. Ananzisha tabia za utamaduni hizi ni muhumi kuelewa siasa na taifa kule Tanzania. Kufanya utafiti, Askew anafanya ethnographia ya muziki, hata alicheza na chama cha taarab. Kita kimoja angeweza kuchofanya tofauti ni kusoma historia za undani zaidi kuunganisha hadithi hii kwa historia za “ritual” kwa upana zaidi.



License

Icon for the Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License

Resources for Self-Instructional Learners of Less Commonly Taught Languages Copyright © by University of Wisconsin-Madison Students in African 671 is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License, except where otherwise noted.