"

Swahili

Matatizo ya Afya- Health Conditions

olanipekun

Learning Objectives

By the end of the lesson, you should be able to:

  1. mention common sicknesses.
  2. use health-related vocabulary in conversation
  3. Talk about signs and symptoms of ailments.

 

Step 1: Review body parts

Step 2: Learn how to ask about someone’s health and possible responses.

Unaendeleaje (leo)? = Nahisi vizuri/Sijihisi vizuri

Note that kuhisi is to feel.

Step 3:

Learn common words associated with health like: dawa -medicine, duka la dawa -pharmacy, hospitalini- hospital, daktari- doctor, mgonjwa- patient, muuguzi- nurse, etc.

Step 4: Study common sickness as they affect different body parts

  1. Homa- fever
  2. Maumivu ya kichwa- headache
  3. Maumivu ya tumbo- stomachpain
  4. Maumivu ya jino- toothpain
  5. Shinikizo- stress
  6. Ugonjwa wa kuhara- diarrhea
  7. Sumu kwenye chakula- food poisoning

Step 5:

Roleplay with your mentor to talk about any sickness for example, the last time you were ill.

Nimekua na maumivu ya …

Nilikuwa na homa kwa…

Ilianza jana/wiki iliyopita

Step 6:

Practice the dialogues below with your mentor, identify and use unknown words.

Dialogue 1

Wema: Nina maumivu ya kichwa

Muuguzi: Yameanza lini?

Wema: Nafikiri yameanza tangu ijumaa iliyopita

Muuguzi: Unapata usingizi wa kutosha?

Wema: Hapana. Siwezi kulala vizuri

Muuguzi: Una shinikizo?

Wema: Ndio, kutoka kazini.

Muuguzi: Inabidi upunzika kwa wiki moja.

(Adapted from Ling)

 

Dialogue 2

Zawadi: Habari za asubuhi daktari?

Daktari: Nzuri mama. Shikamoo

Zawadi: Marahaba

Daktari: Je, una shida gani mama?

Zawadi: Sijisikii vizuri. Ninaumwa kitchwa, tumbo, mgongo na kifua.

Daktari: Tangu limi?

Zawadi: Tangu juzi

Daktari: Unakohoa?

Zawadi: Hapana, sikohoi,

Daktari: Nitakupima kifua. Je, una homa?

Zawadi: Ndiyo, nina homa. Pia ninasikia baridi

Daktari: Je, unatapika?

Zawadi: Hapana, sitapiki. Lakini ninasikia kichefuchefu na kizunguzungu

Daktari: Je, unaharisha?

Zawadi: Siharishi, lakini sipati choo

Daktari: Jana ulikula nini?

Zawadi: Nilikula wa kwa maharage

Daktari: Ulikunywa maji?

Zawadi: Hapana, sikunywa maji wala sijisikii kunywa maji.

Daktari:  Pole mama!

Zawadi: Asante, daktari.

Daktari: Titakupima damu na choo katika maabara. Baada ya kutoka maabara, utaleta majibu halafu nitakuandika dawa

Zawadi: Sawa. Asante datari

(Extracted from Furahia Kiswahili: Kiswahili kwa Wageni)

 

Reference

Baraza la Kiswahili la Taifa (Tanzania). (2014). Furahia Kiswahili: Kiswahili kwa Wageni.

 

License

Icon for the Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License

Resources for Self-Instructional Learners of Less Commonly Taught Languages Copyright © by University of Wisconsin-Madison Students in African 671 is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License, except where otherwise noted.

Share This Book